Msanii nyota wa Tanzania, Abby Chams, ameendelea kuvunja mipaka si tu kwa kipaji chake cha muziki bali pia kwa sauti yake kwenye masuala ya kijamii. Akihojiwa hivi karibuni, Abby alitoa kauli iliyozua mjadala mtandaoni:
“Nadhani hii generation yetu inaongoza kwa kuwa na most toxic men.”
Kauli hiyo imewagusa wengi, hasa wanawake vijana, ambao wameonekana kuunga mkono ujasiri wake wa kulisema wazi jambo ambalo mara nyingi hukwepwa.
Kwa sasa, Abby Chams anatamba na wimbo wake mpya uitwao Hold Me — wimbo wa kimahaba uliojaa hisia, midundo laini, na ujumbe wa mahitaji ya upendo wa kweli. Wimbo huo unaendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki mtandaoni kama vile YouTube, Boomplay na Spotify.
Abby pia alivutia macho ya dunia aliposhiriki kwenye Tuzo za BET, hatua ambayo imezidi kumtambulisha kimataifa kama mmoja wa wasanii wa kike wa Afrika Mashariki wanaochipua kwa kasi ya ajabu.