AJALI YA KUTISHA! MKE WA TAJIRI MAARUFU AMGONGA MREMBO WA MIAKA 24 HADI KIFO


Mamlaka za sheria nchini Italia zimemfungulia uchunguzi Vivian Alexandra Spohr, mke wa Mkurugenzi Mtendaji wa Lufthansa, Carsten Spohr, kwa tuhuma za kumuua mtembea kwa miguu kwenye ajali ya gari na kisha kuondoka nchini.

Vivian anadaiwa kumgonga kwa gari la kifahari aina ya SUV msichana wa miaka 24 aitwaye Gaia Costa, aliyekuwa akivuka barabara kwenye zebra crossing katika mji wa Porto Cervo, Sardinia, Jumanne ya Julai 8. Gaia, aliyefanya kazi kama babysitter, alijeruhiwa vibaya kichwani na alifariki dunia licha ya juhudi za wahudumu wa dharura kumpa huduma ya kwanza kwa zaidi ya dakika 20.

Mke wa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Lufthansa, ambaye ni bilionea, anatuhumiwa kumgonga na gari na kumuua msichana mlezi wa mtoto wakati wa likizo huko Sardinia — kisha kukimbilia  Ujerumani huku uchunguzi ukiendelea.
Picha: Gisela Schober/Getty Images

Mashahidi wanasema kuwa kamera za usalama zilimnasa Gaia akijaribu kuonyesha ishara kwa gari hiyo kabla ya kugongwa. Ripoti za ndani zinaeleza kuwa Vivian Spohr hakuwa amegundua kuwa amegonga mtu hadi alipositishwa na mpita njia. Alipoona hali ya majeruhi, alizimia kwa mshtuko. Vipimo vya pombe na dawa za kulevya vilivyofanywa mara moja vilithibitisha kuwa hakuwa ametumia kilevi chochote.

Baada ya tukio hilo, Vivian aliondoka Sardinia na kurudi Munich, hatua ambayo imezusha maswali kutoka kwa umma na vyombo vya sheria. Waendesha mashtaka wa Italia sasa wamemfungulia uchunguzi kwa kosa la uuaji wa kizembe barabarani (negligent homicide). Mwendesha mashtaka Milena Aucone amemsajili rasmi kama mshukiwa, huku mawakili wake wakithibitisha kuwa anashirikiana kikamilifu na uchunguzi wa mamlaka za Italia.

Taarifa rasmi iliyotolewa kwa niaba yake imesema:

“Vivian Spohr, aliyekumbwa na tukio hili la kusikitisha, anaeleza mshtuko na masikitiko makubwa kuhusu ajali hii nzito.”

Gari lililohusika limekamatwa kwa uchunguzi wa kisayansi, na uchunguzi wa mwili wa Gaia unatarajiwa kufanyika. Hakuna aliyekamatwa kufikia Ijumaa alasiri.

Meya wa Porto Cervo, Gianni Addis, ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Gaia na kumuelezea marehemu kuwa:

“msichana mwenye moyo wa kujitolea, aliyeshiriki kikamilifu katika maisha ya kijamii na utamaduni wa mji wetu.”

Kulingana na European Road Safety Observatory, Italia iliripoti vifo 2,395 vinavyotokana na ajali za barabarani mwaka 2020, na kuifanya iwe katika nafasi ya 11 kwa kiwango cha chini cha vifo kati ya mataifa ya Umoja wa Ulaya.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi