Chelsea Yamtambulisha Kiungo Dario Essugo Kutoka Sporting CP


Chelsea wamethibitisha kumsajili kiungo Dario Essugo kutoka Sporting CP kwa mkataba wa muda mrefu hadi Juni 2033. Klabu hizo mbili zilifikia makubaliano mapema mwaka huu, huku Sporting ikithibitisha kuwa Chelsea imelipa ada ya uhamisho ya €22.3 milioni kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20.

Essugo anajiunga na kikosi cha Chelsea kwa safari ya kuelekea Marekani mwezi huu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya. Msimu uliopita, Essugo alicheza kwa mkopo katika klabu ya Las Palmas na alionyesha uwezo mkubwa licha ya timu hiyo kushuka daraja kutoka La Liga, akicheza mechi 27.

Kwenye historia yake, Essugo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kuichezea Sporting CP alipocheza mechi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 16 na siku 6 tu mnamo Machi 2021. Ameiwakilisha Ureno kuanzia kikosi cha U15 hadi U21.

Inatarajiwa kuwa Essugo atafuatiwa na mshambuliaji wa Ipswich Town, Liam Delap, ambaye tayari amekamilisha vipimo vya afya na kukamilisha usajili wake wa pauni milioni 30.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi