“Mtoto Aliyefariki Miaka 10 Iliyopita Aibuka Hai Geita – Familia Yashindwa Kuamini Macho Yao!” πŸ˜±πŸ§’πŸΎ




 Katika tukio lisilo la kawaida lililotokea katika kijiji cha Nyalubanga, kata ya Lwezela, wilayani Geita, wakazi wamejikuta katika hali ya mshangao na taharuki baada ya mtoto anayesemekana kuwa alifariki dunia miaka kumi iliyopita kupatikana akiwa hai.

Mtoto huyo, anayefahamika kwa jina la Mashaka Kasim, alifariki dunia mwaka 2015 akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi minne kutokana na kile kilichodaiwa kuwa homa kali. Baada ya kifo chake, alizikwa karibu na nyumba ya familia yao na maisha yakaendelea kama kawaida kwa familia ya Mzee Kasim.

Hata hivyo, hali ilibadilika ghafla mnamo tarehe 10 Julai 2025, wakati familia na majirani walipomwona mtoto huyo akionekana waziwazi maeneo ya nje ya nyumba yao – eneo hilo hilo ambalo inasemekana alizikwa miaka kumi iliyopita. Tukio hilo liliwacha jamii nzima ikishangaa na kuanza kujiuliza maswali mazito kuhusu ukweli wa kilichotokea.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyalubanga, Bi. Bahati Fungameza, amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa kwa kuwa mtoto huyo alifariki akiwa bado mchanga, ni vigumu kwa familia na wakazi kuthibitisha kwa haraka ikiwa kweli ni yeye. Hivyo, mamlaka zimechukua sampuli za damu kwa ajili ya vipimo vya kitaalamu ili kufanikisha uchunguzi wa kina na kubaini kama kweli huyo ni mtoto wa familia ya Mzee Kasim.


Kwa sasa, tukio hilo limezua hisia mseto miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho. Wengine wanahusisha hali hiyo na masuala ya imani za kishirikina, huku wengine wakisisitiza umuhimu wa kungojea taarifa rasmi za kitaalamu kabla ya kutoa hitimisho lolote.

Je, inawezekana mtu aliyefariki miaka 10 iliyopita kurudi akiwa hai?
Tunasubiri majibu kutoka kwa wataalamu wa afya na mamlaka husika ili kufahamu ukweli wa tukio hili lisilo la kawaida.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi